Mbivu na mbichi rufaa ya kina Zombe leo

aliyekuwa Mkuu wa Upelelezi Mkoa wa Dar es Salaam (RCO) Kamishna Msaidizi wa Polisi Abdallah Zombe 

Dar es Salaam. Baada ya kimya kirefu, Mahakama ya Rufani leo itatoa uamuzi wa rufaa ya aliyekuwa Mkuu wa Upelelezi Mkoa wa Dar es Salaam (RCO) Kamishna Msaidizi wa Polisi Abdallah Zombe na maofisa wenzake watatu.

Hukumu hiyo itahitimisha mvutano wa muda mrefu wa kisheria kati ya Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP) na maofisa hao.

Wajibu rufani wengine ni Mrakibu wa Polisi (SP) Christopher Bageni, aliyekuwa Mkuu wa Upelelezi Wilaya ya Kinondoni (OC-CID); aliyekuwa Mkuu wa Upelelezi wa Kituo cha Polisi Urafiki, Mrakibu Msaidizi wa Polisi (ASP) Ahmed Makelle na Rajabu Bakari.

Kwa mujibu wa habari zilizoifikia Mwananchi kutoka mahakamani hapo na kuthibitishwa na Msajili wa Mahakama hiyo John Kahyoza, hukumu inatarajiwa kusomwa leo saa sita mchana.
Mpya zaidi Nzee zaidi

Popular Items