VIJANA watano wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) wamepandishwa kizimbani kwenye Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu wakikabiliwa na makosa ya kimtandao ikiwemo kuunga mkono harakati za Umoja wa Kupinga Udikteta Tanzania (Ukuta),anaandika Faki Sosi.
Pia wafuasi hao wamesomewa mashtaka ya kushabikia mauaji ya Polisi wanne waliouawa, Agosti 24 mwaka huu maeneo ya Mbande kwenye tawi la Benki ya CRDB jijini Dar es Salaam.
Washtakiwa hao ni Denis Mtegwa (Injinia), Dennis Temu (Mhandisi), Shakira Ndevu (Mkulima), Juma Mtatuu (Dereva) na Suleiman Nassoro (Fundi Umeme).
Hata hivyo, washtakiwa hao walisomewa mashtaka yao jana kwa nyakati na mahakimu tofauti katika mahakama hiyo.
Mshtakiwa Temu alisomewa shtaka lake mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Emillius Mchauru na Wakili wa Serikali, Salum Mohammed ambapo alidai kuwa mshtakiwa ana kosa moja.
Alidai kuwa Agosti 30, mwaka huu maeneo ya Tabata Bima jijini Dar es Salaam, kupitia mtandao wa Facebook mshtakiwa alilidhalilisha Jeshi la Polisi kwa kuandika,
*Nipo tayari kwa Ukuta, naomba wanikabidhi askari 10 nipambane nao na wakinishinda Mungu anihukumu inatakiwa tupigane nao mkono kwa mkono,”*.
Baada ya kusomewa kosa hilo mshtakiwa alikana, Wakili Mohammed alidai kuwa upelelezi wa shauri hilo bado haujakamilika na anaomba kupangiwa tarehe nyingine.
Mshtakiwa huyo alinusurika kwenda lumande baada ya kutimiza masharti ya kuwa na wadhamini wawili waliosaini bondi ya Sh.milioni tano.Kesi imeahirishwa hadi Oktoba 12, mwaka huu.
Pia mshtakiwa Nassoro alisomewa shtaka lake la kusambaza taarifa za uongo mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Huruma Shahidi.
Wakili Mohammed alidai Agosti 25 mkwa huu maeneo ya Kigogo Dar es Salaam alitumia mtandao wa Facebook kwa kusambaza taarifa za uongo kwa Watanzania dhidi ya Jeshi la Polisi
Inadaiwa aliandika kwamba *“Safi sana aisee naona wangekufa kama 20 hivi, halafu Simon Sirro tumuulize mazoezi wanafanya kwa ajili ya wake zao,”*.
Baada ya kusomewa shtaka hilo, mshtakiwa huyo alikana kuhusika.Hata hivyo alifanikiwa kuachiwa kwa dhama ya kuwa na wadhamini wawili waliosaini bondi ya Sh.laki tano.Kesi imearishwa hadi Septemba 27, mwaka huu.
Pia Injinia Mtegwa alisomewa shtaka lake mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu Yohanna Yongolo na Wakili wa Serikali Bereck Mwakatubi ambapo alidai anakabiliwa na kosa moja.
Inadaiwa Agosti 24, mwaka huu maeneo ya Ubungo External mshtakiwa kupitia mtandano wa WhatsApp alitumia mawasiliano kufanya udhalilishaji kwa kuandika kwamba,
‘JPM Sijui anawaza nini kichwani hata samahani hajui au nilikosea hajui nchi imefika hapa kwa sababu ya mtu mmoja aliyeamua kujilipua ufahamu wake,
Sijaona tatizo kwa hilo ila kwa huyu bwana ‘Misimamo’ ambayo ameisema msinijaribu ili hali kajaribiwa na ubwabwa wa Jubilee kusema siasa si chuki wala upinzanisi audui,
Ajifunze kushindana kwa hoja sio mitutu ya bunduki na mazoezi yasiyo ya kichwa wala miguu ya Polisi,”.
Mshtakiwa mwingine ni Makame na Mtatuu walisomewa mashtaka yao mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Respicius Mwijage ambapo inadaiwa Agosti 24 mwaka huu kwa nyakati tofauti kati Tegeta na Ocean Road jijini Dar es Salaam walisambaza taarifa za kudhalilisha Jeshi la Polisi kupitia WhatsApp.
Inadaiwa Makame alilidhalilisha jeshi hilo ambapo aliandika kuwa ;
Wakati wao wanajiandaa na Ukuta, wao wanajiandaaa na ujambazi safi sana Majambazi,”.
Mtuhumiwa huyo alikana shtaka na kudhaminiwa na mdhamini mmoja aliyesaini bondi ya Sh.milioni mbili.Shauri hilo litatajwa tena Oktoba 4 mwaka huu.
Naye inadaiwa Agosti 24, aliandika ujumbe wenye lengo la kulichafua jeshi la polisi.
Inadaiwa aliandika “Huyu hata akifa ataenda peponi na kufanya mazoezin kote kule wamekufa Mbagala, Mimi nitakuwa wa kwanza kuandamana kule Kahama Septemba mosi kwa ajili ya Ukuta, nitakuwa namba moja kushika bendera ya Ukuta,
Kifo kipo tu usiogope kwani Mawe na Mapanga yameisha,”.
Baada ya kusomewa shtaka lake, alikana na kadhaminiwa kwa bondi ya Sh.milioni mbili iliyosainiwa na mdhamini mmoja.Kesi imeahirishwa hadi Oktoba 27 mwaka huu.