Wahamiaji haramu 72 kutoka mataifa tisa wamekamatwa na idara ya uhamiaji mkoani Mwanza kwa makosa ya kuingia nchini kinyume cha sheria, wakiwemo raia 22 wa Burundi waliotoroka kwenye kambi ya wakimbizi ya Nyarugusu iliyopo mkoani Kigoma.
Afisa uhamiaji mkoa wa Mwanza, naibu kamishina wa uhamiaji Sixtus Nyaki amesema wahamiaji hao kutoka Ethiopia, Burundi, Kenya, Rwanda, Congo DRC, Afrika Kusini, India, Uganda na China wamekamatwa kuanzia Septemba hadi Oktoba mwaka huu katika maeneo mbalimbali ya mkoa huo, baada ya kuingia nchini bila vibali, kuishi na kufanya biashara bila vibali.
ITV imefika katika ofisi za uhamiaji mkoani Mwanza na kushuhudia wahamiaji haramu watatu kutoka Burundi waliokamatwa katika kituo cha mabasi cha Buzuruga, pamoja na wakenya kumi waliokamatwa Sumve wilaya ya kwimba wakifanya kazi bila kibali, ambapo wahamiaji wote wamefikishwa katika mahakama ya hakimu mkazi na kuhukumiwa kifungo cha mwaka mmoja au faini ya shilingi milioni moja, hata hivyo wamelipa faini na wakati wowote watasafirishwa kurejeshwa kwenye nchi zao.
Afisa uhamiaji huyo wa mkoa wa Mwanza, amezitaja sababu kuu za kuingia kwa wahamiaji haramu katika mkoa huu kuwa ni pamoja na mkoa wa Mwanza kuwa na fursa za uvuvi wa Samaki na dagaa visiwani na pia mkoa huo kuwa mojawapo ya vipenyo vya wahamiaji haramu wanaopita nchini wakitokea Ethiopia na Somalia kuelekea Afrika Kusini na vilevile kutafuta ardhi ya malisho ya mifugo na kilimo.