Meli ya MV Songea iliyokuwa ikifanya safari kutoka Tanzania kwenda Malawi yasitisha safari zake.

Meli ya MV Songea iliyokuwa ikifanya safari zake kati ya Tanzania na nchini Malawi imesitisha safari zake nchini Malawi baada ya kupungua kwa abiria wanaokwenda nchini Malawi na mizigo.

Hayo yamebainishwa na kaimu afisa bandari wa bandari ya Mbambabay wilayani Nyasa mkoani Ruvuma Bw. Hemed Ibrahim na kubainisha kuwa safari za kwenda Malawi zimesitishwa kutokana na kupungua kwa abiria na mizigo ya kwenda Malawi na badala yake inafanya safari za Nyasa-Kyela.

Bw. Hemed Ibrahim amewataka wafanyabiashara kutumia usafiri wa meli hiyo ili safari za kwenda Malawi kupitia ziwa Nyasa ziweze kurejea huku diwani wa kata ya Mbambabay Bw. Ajali Hassan akisema kuwa kusitishwa kwa safari ya meli ya MV. Songea nchini Malawi kumefanya maisha ya wilaya ya Nyasa kuwa magumu.

Kwa upande wao wananchi wa wilaya ya Nyasa wanasema kuwa uchumi wao umeyumba kutokana na kusitishwa kwa safari za meli za Tanzania Malawi.
Mpya zaidi Nzee zaidi