Bonanza la Michezo na upandaji Miti Siku ya Uhuru

Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Misungwi awataka Watumishi wa Umma Wilayani humo kuwa Wabunifu na Kuzitumia fursa za Kilimo cha Pamba na Alizeti ili kuleta Maendeleo na kuachana na tabia ya kulalamika .Mkurugenzi huyo Eliurd Mwaiteleke alitoa maelekezo na Maagizo hayo wakati akiongea na wananchi pamoja na watumishi wa umma kwenye bonanza la Michezo mbalimbali liloandaliwa mahusus kwa ajili ya maadhimisho ya miaka 55 ya Uhuru,ambapo wilaya hiyo iliadhimisha kwa kupanda miti na katika maeneo ya taasisi za Shule na Vituo vya kutolea huduma za Afya. Aliwaagiza

Aliwataka watumishi kuhakikisha wanatunza Mazingira kwa kufanya usafi na kupanda miti pamoja na kuwa Waadilifu na wabunifu na kuachana na Vitendo vya Ufisadi katika nyanja zote badala yake wawatumikie Wananchi ili wapate huduma bora na kuwa na maendeleo endelevu ifikapo 2020.

Alibanisha baadhi ya Mikakati ambayo Wilaya imejiwekea ni pamoja na kuhakikisha wanafufua Kilimo cha pamba na tayari mbegu na pembejeo muhimu zishasambazwa kwa wakulima sambamba na kuanzisha Kilimo cha zao la Alizeti ambacho kitainua uchumi wa Wananchi kwa upande wa Mafuta ya Alizeti, na wilaya imeshanunua mbegu Tani 6 ambazo zimeshaanzwa kugawiwa kwa wakulima kwa kila mkopo na wataweza kurejesha baada ya Mavuno.

Mkurugenzi huyo aliwataka pia watumishi wa umma wilayani humo kufanya kazi kwa kuzingatia Sheria, taratibu na kanuni na kuwataka wale wasiokaa katika Vituo vyao vya kazi kuhamia mara moja vinginevyo watachukuliwa hatua za kinidhamu na tayari ameshapata orodha yao.



Mpya zaidi Nzee zaidi

Popular Items