Darassa amedai mwanzo alikuwa akitoa nyimbo zenye ujumbe lakini zilikuwa zikionekana za kawaida.
“Mwanzo nilikuwa nikitoa nyimbo zenye vionjo vyenye ujumbe wa kutosha lakini hazikuwa zikipokelewa sana ila nilipokaa na kufikiria zaidi, nikatambua nini mashabiki wanataka na ndiyo maana muziki wangu upo juu sana tofauti na zamani,” amesema.
Rapper huyo kwa sasa anafanya vizuri na wimbo wa ‘Muziki’ uliogeuka kama wimbo wa taifa kwa sasa.
