Arusha. Wakati Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) mkoani hapa ikivuka lengo kwa kukusanya Sh137 bilioni katika kipindi cha miezi minne, imetakiwa kuwasaidia wenye viwanda kuongeza uzalishaji ili kupata kodi zaidi.
Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Mrisho Gambo alitoa rai hiyo juzi, alipofungua mkutano wa wamiliki wakubwa wa viwanda Kanda ya Kaskazini ulioandaliwa na TRA.
Gambo (pichani) alisema Serikali ya Awamu ya Tano imejipanga kukuza viwanda ili kuinua uchumi, hivyo mamlaka hiyo inapaswa kuwasaidia wenye viwanda kulipa kodi stahiki.
Alisema yamekuwapo malalamiko katika ukadiriaji kodi, hivyo TRA ikae na wafanyabiashara, kuwapa elimu na kuwasaidia ili kuwapunguzia gharama za uagizaji wa malighafi za viwanda vyao.
Kuhusu matumizi ya mashine za kielektroniki, Gambo aliishauri TRA kuwatumia viongozi wa dini kuhamasisha wafanyabiashara kuzitumia kutoa risiti kwa kila anayenunua bidhaa.
Meneja wa TRA Mkoa wa Arusha, Apili Mbaruku alisema katika kipindi cha miezi minne kuanzia Julai hadi Oktoba, wamevuka lengo kwa kukusanya Sh137 bilioni kati ya Sh135 bilioni walizokuwa wamejiwekea lengo.
Mbaruku alisema katika mwaka wa fedha 2016/17 TRA mkoani hapa imepewa lengo la kukusanya Sh413 bilioni.
Meneja wa wateja wakubwa wa TRA makao makuu, Yeremiah Mbaghi alisema mkutano huo ulilenga kutambua changamoto za wafanyabiashara na kuwapa elimu kuhusu sheria mpya ya Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT).
Serikali ya Awamu ya Tano imejipambanua katika sera zake inataka kujenga na kufufua viwanda ili kufikia uchumi wa kati.