Dar es Salaam. Yanga imepigwa faini ya Sh53 milioni wa kosa la kumsajili beki Hassan Ramadhani Kessy huku bado akiwa na mkataba na klabu ya Simba.
Kessy alisajiliwa na Yanga Juni mwaka huu hivyo kuibua mjadala baada ya Simba kupinga jambo hilo kwa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) kwa madai bado ni mchezaji wao halali kwa sababu ana mkataba.
“Klabu ya Yanga inatozwa faini ya Sh3 milioni kwa mujibu wa kanuni na fidia kwa klabu ya Simba ya Sh50 milioni.
“Pia Ofisa wa TFF aliyehusika ama kwa kushirikiana na uongozi wa Yanga au kwa kutochukua hatua stahiki kwa wakati atapelekwa kwenye mamlaka yake ya nidhamu, yaani Katibu wa TFF ili hatua stahiki zichukuliwe dhidi yake,” ilisema taarifa ya TFF kwa vyombo vya habari jana.
Ofisa Habari wa TFF, Alfred Lucas alisema jana kwamba hawezi kumtaja mtu aliyepeleka majina ya Yanga CAF likiwamo jina la Kessy kwa kuwa ni masuala ya ndani ya ofisi.
Hata hivyo, pamoja na kwamba taarifa ya TFF haikumtaja, lakini muidhinishaji mkuu wa masuala yote ya kiofisi kwa mujibu wa sheria ikiwamo kupeleka majina ya timu CAF kwa mashindano ya klabu Afrika, ni Katibu Mkuu wa TFF.
Katibu wa TFF, Celestine Mwesigwa alipopigiwa mara kadhaa jana kuhusiana jambo na hilo, simu yake iliita bila majibu.
Kessy alijiunga na Yanga baada ya kuingia katika mgogoro na klabu yake ya Simba iliyomsimamisha kutokana na madai ya kuwa ‘mnazi’ wa timu hiyo ya Jangwani.
Sakata la Kessy
Mgogoro kuhusu mchezaji huyo uliibukai baada ya kurudisha mpira kwa pasi fupi kwa kipa wake, Vincent Angban na kunaswa na mshambuliaji wa Yanga, Donald Ngoma aliyeukwamisha mpira nyavuni katika mchezo baina ya timu hizo uliofanyika Machi mwaka huu na Simba kufungwa mabao 2-0.
Kutokana na sakata hilo, licha ya Kessy kusajiliwa mwanzo wa msimu na Yanga, ilibidi asicheze baadhi ya mechi za mwanzo kabla ya TFF kumuidhinisha kuwa mchezaji halali wa Yanga na anapaswa kuitumikia timu hiyo wakati suala lake likiendelea kujadiliwa na pande husika.
Hata hivyo, kwa kupitia mawasilisho ya pande zote kwa njia ya mahojiano na vielelezo Kamati ya Katiba, Sheria na Hadhi za Wachezaji imebaini mambo sita yaliyoitia hatiani Yanga.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotumwa jana na TFF kwa vyombo vya habari, ilisema kamati hiyo ilibaini kuwa Kessy alikuwa na mkataba na Simba uliokuwa unamalizika Juni 15 mwaka huu.
Taarifa hiyo ilisema Yanga walikiri mbele ya kamati kupeleka jina la mchezaji huyo kwa Shirikisho la Soka Afrika (CAF) Juni 10 mwaka huu huku mchezaji huyo akiwa ndani ya mkataba na Simba.
“TFF kupitia sekretarieti yake ilikuwa na nafasi ya kuielekeza Yanga hatua stahiki za kuchukua ikiwa ni pamoja na kuwasiliana na Simba kama taratibu zinavyoelekeza. Kama hatua hii ingechukuliwa kwa wakati mwafaka mgogoro huu usingekuwa na sura ya sasa na pengine usingekuwepo.
Ushahidi wa Simba
“Simba walileta machapisho yanayotokana na Mtandao/blogu ya mtu waliyemtaja kuwa ni Bin Zubeiry ukimwonyesha Kessy akiwa na viongozi wa Yanga, wakati mabingwa hao wakionyesha mkataba uliosainiwa na Kessy Juni 20 mwaka huu na hivyo hakukuwa na sababu ya msingi ya kufanya mambo yaliyoainishwa kwenye kipengele cha pili na nne kabla ya kumalizika kwa mkataba kati mchezaji na klabu ya Simba,” ilisema taarifa hiyo.
“Bila kuathiri hadhi ya wanachama wengine wa TFF, klabu ya Simba ina hadhi kubwa kama ilivyo Yanga, hivyo umakini mkubwa unapaswa kutumika katika kushughulikia hadhi hizo ili kuepuka madhara yasiyokuwa ya lazima.”
Kutokana na mambo hayo yaliyoainishwa, kamati hiyo imechukua hatua ya kuipiga faini Yanga ya Sh53 milioni, Simba ikitakiwa kulipwa Sh50 milioni wakati Sh3 milioni zikipelekwa TFF kwa mujibu wa kanuni.
“Kitendo cha Yanga kupeleka jina la mchezaji wa klabu nyingine CAF huku mchezaji huyo akiwa ndani ya mkataba na mwanachama mwingine wa TFF ni kosa kubwa kwa mujibu wa kanuni za ligi kifungu cha 69(5).
“Hivyo wanapaswa kupewa adhabu itakayosababisha wanachama wote kuheshimu nafasi ya TFF kwenye suala la usajili na siyo kuanza kwenda CAF au kwingineko ili kulinda heshima ya soka la Tanzania.
Aveva alonga
Rais wa Simba, Evance Aveva alisema jana kuwa, hawajapata taarifa ya TFF na kwamba wakiipata watakutana na kuitolea ufafanuzi.
“Ndiyo kwanza nasikia hizo taarifa, bado hatujapata rasmi huo uamuzi uliotolewa na TFF kuhusu jambo hilo, hivyo ngoja tutakaa na wenzangu kujadili halafu tutalitolea tamko tutakapopata taarifa kamili,” alisema Aveva.
Kauli ya Katibu Yanga
Katibu wa Yanga, Baraka Deusdedit alisema wamelisikia jambo hilo na wapewe muda wa kujadili kisha watatoa tamko lao kama klabu.
“Ngoja kwanza tuupitie huo uamuzi halafu tutautolea ufafanuzi kama tunakubaliana na adhabu hiyo ama la,” alisema Baraka.
Hata hivyo, Baraka alielezea kushangazwa na moja ya sababu ikiwa ni pamoja na kupeleka jina la Kessy CAF wakati bado ana mkataba na Simba na kusema kuwa wasingeweza kufanya hivyo bila kupitia TFF.