Hospitali kubwa ya kisasa inayojengwa kwa ufadhili wa Shirika la Misaada la Korea – Koica inatarajiwa kufunguliwa mwezi Februari mwakani baada ya ujenzi wake kukamilika ambapo hivi sasa imefikia asilimia 80.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Paul Makonda amefanya ziara katika Hospitali hiyo iliyopo Chanika jijini humo ambayo ni mahsusi kwa ajili ya kutoa huduma za mama na mtoto, upasuaji, huduma za dharura ikiwa ni pamoja na kuhudumia wagonjwa mbali mbali zaidi ya elfu moja kwa Siku.
Amesema kukamilika kwa Hospitali hiyo kutasaidia kupunguza msongamano katika Hospitali za Amana na Temeke kwa kuwa kutakuwa na madaktari Bingwa kutoka hapa nchini pamoja na wale watakaotoka Korea ambapo pia wataendesha mafunzo maalum hapa nchini.
Makonda amesema pamoja na ujenzi wa hospitali hiyo inayotarajiwa kuzinduliwa na Rais Dk.Magufuli lakini hospitali nyingine zinatarajiwa kujengwa kwenye wilaya mpya za Kigamboni na Ubungo, lengo likiwa kuongeza kasi ya upatikanaji wa huduma za afya katika jiji la Dar es salaam na kuondoa Msongamano kwenye Hospitali za Rufaa.