Jeshi la polisi limekili kuhusika na mauaji ya watu wawili kwa kuwapiga risasi, tukio lililotoke kisaki kijiji cha Kituoni mkoani Morogoro kwa madai ya wananchi walikua wanazuia kukamatwa kwa watuhumiwa wa makosa makubwa waliopo katika eneo hilo.
Akiongea na waandishi wa habari kamanda wa polisi mkoa wa Morogoro Urlich Matei amesema wakati askali wakitekeleza majukumu yao ya kukamata watuhumiwa hao wa makosa makubwa ndipo wananchi walikusanyika na kufunga barabara kwa magogo na kurusha mawe jambo ambalo jeshi la polisi lilipiga risasi 22 juu kati ya hizo zilisababisha watu wawili kufariki dunia na mmoja kujeruhiewa na kulazwa katika hospitali ya mkoa wa Morogoro.
Channel Ten ilifika katika hospitali ya mkoa wa morogoro ambapo mganga mfawidhi wa hospiatal ya mkoa Francis Semwene amekanusha kuwepo kwa majeruhi katika hospitali hiyo huku wananchi wa kisaki wakilalamikia jeshi la polisi kufanya operesheni hiyo bila kushirikisha serikali ya kijiji.
Source: Channel Ten