Ama kweli dunia rangi rangile kina kunapokucha uvumbuzi na ugunduzi unazidi kushika hatamu, kuna vitu vingine ukihadithiwa ama kubahatika kukutana navyo utabaki kinywa wazi.
Baada ya gari linalopaa kama ndege kugunduliwa hivi karibuni pamoja na roboti linalohudumia wagonjwa katika moja ya hospitali huko ughaibuni sasa Chuo Kikuu cha Stanford cha Marekani kimevumbua kitambaa kinachoweza kurudisha mwanga wa jua na kupitisha joto la mwili kwa ufanisi mkubwa ambapo mtu akivaa nguo iliyoshonwa kwa kitambaa hiki atahisi baridi zaidi.
Naibu Prof. Cui Yi wa Idara ya Sayansi ya Malighafi na Uhandisi ya Chuo Kikuu cha Stanford anayeongoza utafiti huo alifahamisha kuwa, malighafi ya kitambaa hiki ni Polyethylene yenye matundu mengi madogo madogo yenye kipenyo cha nanomita kadhaa.
Kabla ya hapo, malighafi hii ilitumiwa katika uzalishaji wa betri za Li-ion. Joto la mwili wa binadamu linatolewa kwa njia ya mwanga wa infrared na malighafi hii inaweza kupitisha mwanga wa infrared bila vizuizi vyovyote.
Aidha, matundu madogo madogo yanasaidia kupitisha hewa na unyevu. Majaribio yanaonesha kuwa mtu akivaa nguo iliyoshonwa kwa kitambaa hiki, joto la mwili wake litaongezeka kwa nyuzi 0.8 tu lakini akivaa nguo ya kitambaa cha pamba, joto litaongezeka kwa nyuzi 3.5 na akivaa nguo ya kitambaa cha Polyethylene ya kawaida, joto litaongezeka kwa 2.9. Hii inamaanisha kuwa mtu anayevaa kitambaa cha aina mpya atahisi baridi zaidi kuliko vitambaa vingine.
Prof. Cui Yi alisema malighafi hii inatazamiwa kutumiwa kwa wingi katika utengenezaji wa nguo, hasa nguo za michezo, na kikundi chake kitaendelea kutafiti na kuvumbua kitambaa chenye ubora zaidi.