Zaidi ya watu 200 wamekosa makazi na mmoja kujeruhiwa baada ya nyumba zaidi ya 50 kubomolewa na nyingine kuezuliwa paa zake kufuatia mvua iliyonyesha usiku wa kuamkia jana katika vijiji vya Mpwapwa na Jangwani vilivyoko katika wilaya ya Sumbawanga Mkoani Rukwa.
Katika maafa hayo ya mvua, kijana wa miaka sita alijeruhiwa kichwani na kupoteza fahamu alifikishwa katika zahanati ya kijiji Mpwapwa na baadae hospitali ya Mkoa ili kunusuru maisha yake, uongozi wa kijiji unaomba misaada ya kibinadamu ya kuwasitiri waathirika katika wakati huu mgumu.