Madiwani Geita walalamikia Polisi Kwa kuwakamata wafanyabiashara na kumwaga mali zao

Madiwani wa Halmashauri ya Wilaya ya Geita vijijini na Geita mjini wamelalamikia jeshi la Polisi wilayani Geita kwa kuwakamata wafanyabiashara na kumwaga mali zao kwa kile kinachodaiwa kuzuia uhalifu.

Wametoa lawama hizo mbele ya Mkuu wa Wilaya hiyo Herman Kapufi, kwenye kikao kilichowakutanisha Madiwani na Maafisa wa Halimashauri hizo lengo likiwa ni kuzungumzia ziara ya Mkuu wa wilaya huyo nchini China.

Kwa upande wake, Mbunge wa Geita Mjini, Constantine Kanyasu ameshauri utaalamu zaidi wa kipolisi kutumika katika kuwadhibiti majambazi na vibaka, huku Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mji wa Geita Leonard Bugomola akisisitiza wafanyabiashara wanaokamatwa na kusumbuliwa wana leseni halali za biashara.

Akijibu malalamiko hayo, Mkuu wa Wilaya ya Geita Herman Kapufi ameahidi kulifuatilia suala hilo ambapo amesisitiza askari Polisi hawana dhamira mbaya.
Mpya zaidi Nzee zaidi