Mshambuliaji wa kimataifa anayeichezea Klabu ya Super Eagles ya nchini Afrika kusini Mtanzania Uhuru Suleiman amesema, kufanya vizuri au kutofanya vizuri kwa vilabu inategemea na mfumo wa soka la Tanzania
hususani kwa upande wa wadhamini ndani ya vilabu.
Akiongea na EATV Uhuru amesema vilabu vinapopata wadhamini vinakuwa na uwezo mkubwa wa kufanya vizuri ndani ya Ligi na hata mashindano mbalimbali makubwa.
"Wachezaji wa kigeni tunaangaliwa sana kwa sababu inapofikia timu yako imefanya vibaya hawamuulizi mchezaji ambaye ni mzawa bali unafuatwa wewe na kuulizwa kwanini timu imefanya vibaya suala linalofanya tuzidi kupambana," amesema Uhuru.
Uhuru ameongeza kuwa vilabu vingi vimekuwa vikiangalia wachezaji wa ndani pekee vikiamini wao ndio wenye mamlaka ya kuifikisha timu sehemu nzuri bila ya kufikiria ya kuwa wachezaji wote wanamamlaka ya kucheza kwa bidii ili kuiweka timu katika sehemu nzuri.