Mahakama Ilala Yatupilia Mbali Pingamizi La Kuzuia Mkutano Wa Simba Jumapili

Rais wa simba, evans aveva akiwasalimia wanachama wa klabu hiyo.

Mahakama ya Wilaya ya Ilala imetupilia mbali pingamizi la baadhi ya wanachama wa klabu ya Simba waliotaka kuzuiwa kwa mkutano uliopangwa kufanyika Jumapili.

Mahakama hiyo imewaona waliopinga kuwa hawana hoja ya msingi na kupitisha mkutano huo ufanyike Jumapili.

Mkutano huo umepangwa kufanyika Jumapili kwa lengo la kujadili masuala kadhaa ya klabu hiyo likiwepo lile la mabadiliko.

Tayari mfanyabiashara bilionea, Mohammed Dewji maarufu kama Mo amesema yuko tayari kutoa Sh bilioni 20 na kuwekeza Simba.

Mpya zaidi Nzee zaidi

Popular Items

Kilimo cha Bamia