Watuhumiwa mauaji ya Bondia Mashali wafikishwa mahakamani kwa mara ya kwanza

Usiku wa kuamkia October 31 2016 Tanzania ilimpoteza bondia maarufu wa ngumi za kulipwa  Thomas Mashali ambapo ilielezwa kuwa Marehemu Mashali alifariki kwa kushambuliwa na watu baada ya kusingiziwa ni mwizi na watu ambao aligombana nao maeneo ya Kimara Dar es salaam.

Leo December 8 2016 kwa mara ya kwanza watuhumiwa saba wa mauaji ya bondia huyo wamefikishwa mahakama ya hakimu mkazi Kinondoni na kusomewa shitaka la mauaji, kesi hiyo itatajwa tena December 20 2016 na watuhumiwa wote wamerudishwa rumande.
Mpya zaidi Nzee zaidi

Popular Items

Kilimo cha Bamia