INASHANGAZA kuona mchezaji wa kikosi cha kwanza na nahodha wa timu hatakiwi na timu yake! Kushindwa kuwasaini mikataba mipya wachezaji wake, mlinzi wa kati Mganda, Juuko Murshid, mshambulizi Ibrahim Ajibu na nahodha Jonas Mkude ni muendelezo wa kuanguka ndani ya uwanja kwa mabingwa wa zamani wa Tanzania-Simba SC.
Huwezi kusema mnajenga timu mpya ya kutwaa mataji wakati kila msimu mnapoteza wachezaji muhimu kikosini mwenu. Ndani ya misimu mitano iliyopita Simba imewapoteza baadhi ya wachezaji wake muhimu, hasa wale wazawa. Rejea kikosi kile cha U20 kilichokuwa chini ya kocha Suleimani Matola mwaka 2012.
Arsenal ya England ipo katika presha ya kuwapoteza wachezaji wake muhimu-mshambulizi, Alexs Sanchez na kiungo ‘maestro,’ Mesut Ozil ambao mikataba yao inaelekea mwishoni na wamegoma kusaini mikataba mipya na wakali hao wa London hadi pale watakapoongeza kiasi cha pesa wanachokitaka.
Kuna mambo ya kujifunza hapa, Kwanza ni maslahi-Arsenal inafahamu umuhimu wa wachezaji hao katika timu yao ndiyo maana wamekuwa katika mazungumzo ya kuhakikisha wanawaongezea mikataba, lakini wachezaji hao wanahitaji zaidi ya kile ambacho Arsenal wanataka kuwapa.
Arsenal wana ‘kitu kidogo’ na wachezaji wanaona huu ni wakati wao wa kupata ‘kitu kikubwa’ zaidi vinginevyo wataenda sehemu nyingine ambako watalipwa zaidi ya kile ambacho Arsenal inataka kuwalipa.
Pili, Kutumikia mkataba wao wa sasa- Sanchez na Ozil wamekuwa katika viwango vya juu msimu huu na wameendelea kupambana kwa nguvu zao, maarifa na akili zao ili kuisaidia timu yao.
Uwajibikaji wao unaendelea kuisaidia Arsenal, pia viwango vyao vinaendelea kupandisha thamani yao. Licha ya kutofautiana katika mazungumzo ya kusaini mikataba mipya kila upande umeendelea kuwa na heshima dhidi ya upande mwingine. Klabu haiwasemi vibaya wachezaji hao, na wachezaji wameendelea kucheza kwa ubora zaidi.
Hivi ndivyo wanavyopaswa kuishi Simba na wachezaji wao ambao wamegomea mikataba mipya hivi sasa. Hata kama wataondoka klabuni hapo mara baada ya kumalizika kwa mikataba yao ya sasa, Mkude, Ajibu na Juuko wanapaswa kuendelea kufanya kazi yao kwa nguvu, akili na maarifa zaidi kwani hiyo ndiyo njia sahihi ya kuimarisha soko lao.
Simba pia wanapaswa kufahamu kufeli kwa harakati zao za kuwasaini wachezaji hao kusiwe sababu ya kuwasema vibaya vijana hao bali wanachopaswa ni kuendelea kuwaheshimu huku wakiendelea kuzungumza nao, ikishindikana kila upande uwe na amani hata kama upande fulani hautaridhika.