Mongela Atinga Mitaani Kuhimiza Usafi wa Jiji la Mwanza

 Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, John Mongela akikatiza katika mitaa mbalimbali ya Jiji la Mwanza kuhimiza usafi.
 Mhe. John Mongela akitoa maelezo kuondoa vitu vilivyowekwa nje ya duka la mkazi wa Mwanza.
 Wakazi wa Mwanza eneo la soko kuu wakiondoa uchafu katika mtaro uliopo eneo hilo.
 Zoezi la kusafisha Jiji la Mwanza likiendelea.
Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, John Mongela ametembea mitaa mbalimbali ya Jiji la Mwanza kuhimiza watu kufanya usafi katika maeneo wanayofanyia kazi pamoja na kutoa muongozo wa namna wafanyabiashara watakavyoendesha biashara zao.

Ziara hiyo imefanyika baada ya kumaliza zoezi la kuondoa wafanyabiashara wadogo wadogo (machinga) katika maeneo yasiyoruhusiwa na kuwapeleka maeneo mbalimbali ambayo yalitengwa kwa ajili ya wafanyabiashara hao.

Katika ziara hiyo iliyokuwa imeambatana na viongozi mbalimbali wa serikali walipita maeneo ya Makoroboi, Liberty, soko kuu na daraja la wamasai ili kujionea hali halisi ilivyo baada ya kuondolewa kwa machinga katikati ya mji.

Source: Global Publisher
Mpya zaidi Nzee zaidi

Popular Items