Moro yakabiliwa na uhaba wa damu

MKOA wa Morogoro unakabiliwa na upungufu wa akiba ya damu salama, hasa katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa huo.

Hali hiyo imeelezwa inatokana na wananchi kushindwa kujitolea damu kwa wingi na kusababisha upungufu huo, hivyo kuathiri utoaji wa huduma ya haraka kwa wahitaji wa damu, hasa wajawazito, watoto na majeruhi wa ajali.

Mganga Mkuu wa Mkoa, Dk Frank Jacob aliyasema hayo juzi alipozungumzia mkakati wa kampeni ya uchangiaji damu salama unaofanyika katika Manispaa ya Morogoro kwa muda wa siku tano kuanzia Desemba 20, mwaka huu.

Alisema mahitaji ya damu kwa mwezi kimkoa ni chupa 2,266, lakini kiasi kinachopatikana hadi sasa ni chupa 924 ambacho hakitoshelezi.

Kaimu Mratibu wa damu salama mkoani Morogoro, Chiku James alisema uhaba huo umeongeza zaidi kati ya Novemba na Desemba mwaka huu kutokana na wanafunzi wa sekondari na vyuo Ambao ni wachangiaji wakubwa wa damu kuwa wako likizo
Mpya zaidi Nzee zaidi

Popular Items