Mtengenezaji wa pombe haramu adakwa Rombo



Rombo. Mapipa 13 ya pombe ya kienyeji aina ya Iyembe yamekamatwa na kumwagwa wilayani hapa Mkoa wa Kilimanjaro.

Mkuu wa Wilaya ya Rombo, Agnes Hokororo alisema katika operesheni ya kukamata pombe haramu iliyofanyika jana, mtu mmoja anayedaiwa kuzitengeneza pia alikamatwa.

Alisema mtuhumiwa huyo alikamwatwa akiwa na vifaa vya kutengeneza pombe hiyo na malighafi zikiwamo ndizi, amira na sukari vilivyokuwa nyumbani kwake.

Ofisa Afya Wilaya ya Rombo, Mathias Bumbuluka alisema pombe hiyo imekuwa ikisababisha watumiaji kuharisha na wengine kuvimba mwili.

Mpya zaidi Nzee zaidi