John Glenn akijiandaa kusafiri kwenda angani enzi za uhai wake
Mwanaanga wa kwanza wa Marekani kuizunguka dunia kupitia mzingo wake, John Glenn amefariki dunia akiwa na miaka 95.
Glenn aliwahi kutunukiwa tuzo ya dhahabu (Congressional Gold Medal) na Rais Barack Obama, mwaka 2011. Lakini pia mwaka 1998 aliwahi kuweka rekodi ya kuwa mtu wa kwanza mwenye umri mkubwa kwenda angani akiwa na miaka 77.
John anatarajiwa kuzikwa katika makaburi ya Arlington, Virginia.
