Mwasiti ajibu skendo ya kunyanganywa gari

 Mwasiti

Mkali wa bongo fleva kwa akina dada, mrembo Mwasiti, amegoma kunyoosha maelezo kuhusu skendo inayomkabili ya kunyanganywa gari aina ya Benz alilokuwa akilitumia, na kusema hataki kulizungumzia suala hilo.

Akipiga story na eNewz, Mwasiti amesema anawashangaa wanaozungumzia maisha yake hususani gari hiyo huku wakiwa hawajui gari lile ni la nani na yeye alikuwa akilitumia kama nani
“Hapana sijui hata unazungumzia gari gani na mimi sitakagi kuongelea personal life kwenye media sijawahi hata siku moja na sitowahi” Amesema Mwasiti ambaye amewahi kutamba na ngoma kama 'Kisa Pombe' na 'Hao' na pia ni kati ya wasanii wa kike wenye sauti nzuri na wanye uwezo mkubwa wa kuimba.

Mwasiti sasa hivi amerudi tena kwenye game ya bongo fleva na wimbo mwingine unaokwenda kwa jina la 'Kaa nao' ambapo kwa sasa amepata menejimenti au uongozi mpya ambao utakuwa unamsimamia yeye na kazi zake.
Mwasiti akiwa ndani ya studio ya EA Radio

Pia Mwasiti ameeleza kufurahia kupata  menejimenti na amesema yuko kibiashara zaidi na anaamini kupitia menejimenti hiyo kazi zitakuja nyingi na nzuri kwa kwamba video ya wimbo wake itatoka Januari mwaka 2017.

“Kwa sasa nimepata menejimenti mpya ambayo itakuwa inasimamia kazi zangu na watu hao kuna msanii pia mkubwa sana hapa Tanzania ndiyo wanamsimamia, sasa hivi nimekaa kibiashara zaidi na wao wako tayari kunisimamia. Nimefurahi sana kwa sababu mpaka sasa hivi nimewaona kama ni watu ambao wako serious na kazi na nimependa wanavyonihandle wanataka kujua ratiba yangu ya siku nzima pia hata ukiwa studio wanakuwa na wewe na kukupa idea , wameinvest na wao ndio wanafanya kila kitu”
Mpya zaidi Nzee zaidi

Popular Items