Rapa Darassa
Msanii wa bongo fleva Mwasiti ambaye kwa sasa anafanya vizuri na wimbo wake 'Kaa nao' amefunguka na kusema kuwa Rapa Darassa kidogo kupitia wimbo wake wa 'Muziki' amewapa baadhi ya wasanii presha.
"Darassa amefanya kazi nzuri ambayo watu wengi hawakuitegemea kitu alichofanya Darassa angefanya moja kati ya wasanii wetu ambao tunasema ni wasanii wakubwa kingeonekana ni kitu cha kawaida sana. Lakini kwa kuwa Darassa alikuwa wakifanya vitu vyake hivi hivi mdogo mdogo watu walikua wanachukulia poa lakini kwa sasa kwa kuwa kimekua kitu kikubwa kidogo amewapa watu presha". Alisema Mwasiti
Mbali na hilo Mwasiti alisema wimbo wa Darassa ni changamoto kwa wasanii ambao wanafanya muziki ambao Darassa anafanya lakini si kwa wasanii wa kuimba kwani hao si washindani wake.
"Mimi hawezi kunipa presha sababu mimi sifanyi muziki wa Darassa ila wasanii wanaofanya muziki ambao Darassa anafanya ndiyo inawezekana saizi wanasumbuliwa na BP, mimi na muziki wangu ambao nauheshimu sana umenipa 'Fun base' kubwa sana" alisema Mwasiti
