Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli, amewaapisha viongozi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi, Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma na Majaji wa Mahakama ya Rufani aliowateua jana tarehe 22 Desemba, 2016.

Rais Magufuli akimuapisha Jaji Semistocles Simon Kaijage kuwa Mwenyekiti wa NEC
Hafla ya kuwaapisha viongozi hao imehudhuriwa na Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa, Jaji Mkuu wa Tanzania Mhe. Mohamed Chande Othman, Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Utumishi na Utawala Bora Mhe. Anjellah Kairuki, Mwanasheria Mkuu wa Serikali Mhe. George Mcheche Masaju na Viongozi wengine mbalimbali.
Walioapishwa ni Mhe. Mhe. Jaji Semistocles Simon Kaijage aliyeapishwa kuwa Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), Mhe. Jaji Mstaafu Hamid Mahmoud Hamid aliyeapishwa kuwa Makamu Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) na Jaji Mstaafu wa Mahakama ya Rufaa, Mhe. Jaji Harold Reginald Nsekela aliyeapishwa kuwa Kamishna wa Maadili katika Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma. Viongozi hawa watashika nyadhifa hizo kwa kipindi cha miaka 5.
Rais Magufuli akimuapisha Jaji Harold Reginald Nsekela kuwa Kamishna wa Maadili
Kwa upande wa Majaji walioapishwa kuwa Majaji wa Mahakama ya Rufani ni Mhe. Jaji Rehema Kiwanga Mkuye, Mhe. Jaji Sivangilwa Sikalalilwa Mwangesi na Mhe. Jaji Dkt. Gerald Alex Mbonimpa Ndika, Mhe. Jaji Jackobs Casthom Mwatebela Mwambegele.

Rais Magufuli akimuapisha Jaji Mstaafu Hamid Mahmoud Hamid kuwa Makamu Mwenyekiti wa NEC
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Kassim Majaliwa wakiwa katika picha ya pamoja na Mwenyekiti mpya wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) (wakwanza kushoto) na aliyekuwa Mhe. Jaji Mstaafu Damian Lubuva aliyemaliza muda wake.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Kassim Majaliwa wakiwa katika picha ya pamoja na Majaji wa Mahakama za Rufani leo Ikulu Jijini Dar es Salaam

