Rais JOHN POMBE MAGUFULI,leo ameweka hadharani kwanini aliamua kufuta shamrashamra za Miaka 54 ya Uhuru wa Tanzania Bara ikiwamo gwaride la maadhimisho hayo na kusema kuwa ataendelea kuipa umuhimu na heshima siku hiyo.
Dokta Magufuli katika kile ambacho hakikutarajiwa kufuatia utaratibu wa miaka yote wa Marais waliomtangulia kutozungumza na Taifa baada ya gwaride la maadhimisho,ameamua kuvunja ukimya na kuwaambia Wananchi kuwa alichukua maamuzi hayo kufuatia kuwa na siku chache madarakani huku akiwa hajaunda baraza la mawaziri lakini pia ukubwa wa gharama za shamrashamra zilizofikia shilingi bilioni 4 na kuwanufaisha wachache.
Aidha Dokta Magufuli,aliyewaomba radhi Wananchi kwa kitendo chake cha kuelekeza fedha hizo kutengeneza na kupanua baraba ya Ali Hassan Mwinyi,amesema,amezirejesha sherehe za mwaka huu kwakuwa gharama zake ni ndogo na kuondoa alichosema matumizi yakiwemo ya chakula na dhifa ya kitaifa.
Katika hatua nyingine,Dokta Magufuli,amewaambia wanachi kuwa gwaride la maadhimisho ya miaka 55 ya uhuru wa Tanzania Bara,huenda likawa la mwisho kwani kuanzia mwakali litahamia Dodoma,aidha amekiri kuwa licha ya mafanikio yaliyopatikana,bado kuna changamoto ikiwamo za rushwa,Ufisadi,wanafunzi hewa,wafanyakazi hewa na huduma za Elimu na afya.
Awali Rais Magufuli,aliyewasili uwanjani hapo majira ya saa 3 na dakika 55 na kuondoka saa saa 7 na dakika 21,na kupokea salamu ya Rais saa 4 kamili kutoka kwa gwaride la Gadi kumi za Vikosi vya ulinzi na usalama,likiongozwa na Luteni Kanali Makanya Elias,alikagua gwaride hilo,lililoambatana na mizinga 21 saa 4 na dakika10 sambamba na Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na usalama,na saa 4 na dakika 16,aliwavunja mbavu wanachi waliohudhuria uwanjani hao kwa kucheza gwaride kama askari.