Sababu iliyopelekea mchezo wa Sassuolo vs KRC Genk ya Samatta kuahirishwa

Mchezo wa mwisho wa Kundi F wa Europa League kati ya timu ya Sassuolo ya Italia ambayo ilikuwa icheze dhidi ya KCR Genk ya Ubelgiji inayochezewa na mtanzania Mbwana Samatta, mchezo umeahirishwa hadi Ijumaa ya December 9 Saa 14:30 mchana kutokana na hali ya hewa.

Mchezo huo ambao Mbwana Samatta kapangwa kuanza, umeahirishwa kwa sababu ya ukungu uliosababisha watu wasionane uwanjani, ikumbukwe kuwa KRC Genk anacheza mchezo huu kukamilisha ratiba lakini tayari ameshafuzu hatua inayofuata.
Mpya zaidi Nzee zaidi

Popular Items