Serikali imesema baadhi ya wafanyabiashara wasio waaminifu wamekuwa wakidanganya wa bei halisi ya bidhaa wanazoziingiza nchini hasa nguo ili kukwepa kodi na kwamba wataoendelea na tabia hiyo watajuta kufanya hivyo.
Waziri wa viwanda, biashara na uwekezaji Charles Mwijage amesema hayo wakati akifungua maonesho ya viwanda vya ndani na kusema kuwa wanaofanya hivyo watashughulikiwa huku akitoa wito wa kuanzishwa kwa viwanda vingi vya ndani kama njia ya kukabiliana na uingizaji wa bidhaa kutoka nje ya nchi.
Naye kaimu mkurugenzi mkuu wa mamlaka ya biashara ya nje Edwin Rutegeruka amesema katika maonesho hayo wenye viwanda vya ndani wameweza kujifunza wenyewe kwa wenyewe kuhusiana na utengenezaji wa bidhaa bora kauli iliyoungwa mkono na baadhi ya waoneshaji.