Siku mbili baada ya Rais John Pombe Magufuli kuiagiza wizara ya nishati na madini kusitisha zoezi la kuwahamisha wachimbaji wadogo wa Dhahabi katika kijiji cha Nyaligongo kata ya Mwakitolyo wilayani Shinyanga wachimbaji hao wameitaka serikali kuweka utaratibu mzuri utakaowawezesha kulipa kodi ya serikali ili nao wachangie katika juhudi za kukuza uchumi wa nchi.
ITV ilifika katika kijiji cha Nyaligongo eneo linalisadikiwa kuwa na wachimbaji wadogo wa dhahabu zaidi ya elifu saba na kukuta shamrashamra hoihoi vifijo na nderomo zikitawala kila pande za eneo hilo na baada ya muda wachimbaji hao wakakutanika pamoja na kutoa ujumbe wao kwa rais John Pombe Magufuli.
Nao baadhi ya viongozi wa wachimbaji wadogo wa Dhahabu katika eneo hilo la Nyaligongo wameitaka serikali kupitia mamlaka ya mapato Tanzania (TRA) kufika na kutoa semina elekezi kwa wachimbaji juu ya ulipaji wa kodi kwakuwa wako tayari kufanya hivyo tangu awali huku wakidai kuwa serikali imekuwa ikipoteza mapato makubwa kutokana na wachimbaji wadogo nchini kutimuliwa kila wanapogundua eneo lenye madini.