Taa ya kuchaji yateketeza mali za Sh1.4 milioni

Sengerema. Taa ya kuchaji ambayo pia inatumia mwanga wa jua iliyochwa kibandani ikichajiwa imelipuka na kuteketeza mali za Sh1.4 milioni mjini Sengerema.

Hata hivyo, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza, Ahmed Msangi alisema taarifa za tukio hilo zilikuwa hazijafika ofisini kwake na kuahidi kufuatilia.

Mmiliki wa kibanda hicho, Joseph Machela alisema alipofunga biashara saa tatu usiku juzi, aliacha taa hiyo ikichaji lakini ilipofika saa 12:45 asubuhi alipokea simu kuwa kibanda chake kinateketea kwa moto.

Mwenyekiti wa Mtaa wa Migombani mji wa Sengerema, Jane Msoga alisema aliitwa nyumbani kwake na wananchi baada ya kuona moshi ukifuka kwenye kibanda hicho lakini juhudi za kuuzima kuokoa bidhaa ziligonga mwamba.

Diwani wa Nyampulukano, Emmanuel Munwanis alisema juhudi zao zilikwamishwa na zana duni walizotumia kuokoa mali kulinganisha na ukubwa wa moto.
Mpya zaidi Nzee zaidi