F Vijana watakiwa kujitupa huku | Muungwana BLOG

Vijana watakiwa kujitupa huku

Tokeo la picha la kundi la vijana

Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya maendeleo ya Kilimo nchini Francis Assenga amewashauri vijana kujikita katika masuala ya kilimo badala ya kuchagua kazi.

Akizungumza katika kilele cha kongamano la fursa lililoandaliwa na Umoja wa Mataifa,  Assenga alisema benki hiyo imewekwa madhubuti kwa ajili ya kutoa mikopo kwa vijana walio na ari na moyo wa kuleta mabadiliko katika jamii.

"Wengi wamekua wakichagua kazi na wengi wao hawapendi kufanya mambo ya kilimo lakini ni ukweli usiopingika kuwa kilimo ndio sekta ilio na fursa nyingi" ,alisema.


Alisema kuwa kijana akiwa na mawazo makini yenye tija ni rahisi kupata fedha.

"Tatizo wengi wamejikita kulalamikia mambo ya mitaji wewe andaa wazo kwanza," alisema.

Pia katika kongamano hilo Mkuu wa mkoa wa Iringa Richard Kasesela aliwataka vijana kupangilia matumizi yao ya fedha na kuacha tabia ya kutumia fedha kwa matumizi yasiyo  na manufaa.

"Ili ufanikiwe ni muhimu kuhakikisha fedha yako unaitumia vizuri sio unahonga tu bila sababu" alisema na kuongeza:

“Kijana ni muhimu kuwa mthubutu na kuhakikisha haukati tamaa katika mambo unayoyafanya.”

Kwa upande wake Mzungumzaji  Nickson Simon (Nick wa pili) amesema dhana ya kuamini kuwa ujana ni umri imepitwa na wakati badala yake watu watambue kuwa kijana ni uwezo mzuri wa kufikiri bila kujali  umri.


"Kijana ni uwezo wa akili kimaarifa ambayo huwezesha kutafutia ufumbuzi mbalimbali unaweza kujihisi kijana lakini kulala kwa akili yako ukawa mzee" alisema.