Watanzania tuisapoti 'Hapa Kazi Tu' - Askofu

Askofu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Dayosisi ya Kaskazini Magharibi Dkt. Abednego Keshomshahara amewaasa watanzania kufanya kazi kwa bidii ili kuinga mkono kaulimbiu ya 'Hapa Kazi Tu'

Askofu Abednego ametoa wito huo leo Mjini Bukoba katika ibada ya Sikukuu ya Krismasi kitaifa iliyofanyika katika Kanisa Kuu la Kiaskofu, Usharika wa Bukoba Mjini, ambapo amesema sikukuu hii inawakumbusha watanzania kukumbuka kufanya kazi huku wakimuomba Mungu badala ya kutegea maombi pekee pasipo kufanya kazi.

Amewataka washarika na wakristo wote Tanzania kutoyumbishwa na mahubiri yanayowashawishi kutofanya kazi na kutegemea miujiza huku akitolea mfano baadhi ya madhebu ambayo huaminishana kuwa wanaweza kufunga bila kula chochote kwa muda mrefu ili Mungu awatendee miujuiza.

"Tukifanya kazi kwa bidii tunakuwa pia tunaendana na kaulimbiu ya taifa ya Hapa Kazi Tu.....kuna wengine wanaamini wakifunga na kufanya maombi bila kula wala kufanya kazi wataweza kuishi, kwa mfano kuna mtu alifunga akaacha kula mwisho akasababisha mauti"

Pia amesisitiza wazazi na walezi kuitumia Sikukuu hii kutambua umuhimu wa elimu na kuwapeleka watoto shule "Wanaowazuia watoto wao kusoma eti kwa sababu ya dini, wanataka waombe tu, hiyo hata maandiko yanakataza, maandiko yanasema tafuteni nanyi mtapata" Amesema
Mpya zaidi Nzee zaidi