Wakati waislamu duniani kote wakiendelea kusherehekea Sikukuu ya Maulid ya kuzaliwa kwa mtume wao Mohamed S.W.S,wito umetolewa kwa waislamu na wasio waislamu kuendelea kudumisha umoja wa kitaifa ikiwemo kuheshimu haki za kila mmoja bila kujadi dini kama mafundisho ya Mtume Mohamed na Quran Tukufu yanavyosema.
Sheikh wa mkoa wa Dar es salaam Alhadi Musa Salum katika mahojiano na ITV amesema katika kusherehekea sikukuu hii ya Maulidi waislamu wanakumbushwa kuishi kulingana na mafundisho ya Mtume Mohamad alivyofundisha katika Quran Tukufu kwa kutenda mema kwa kila mtu na kuheshimu haki za kila mmoja bila kuangalia tofauti ya dini wala kabila.
Pia amewataka watanzania wote,waislamu na wasio waislamu kuendelea kudumisha umoja wa kitaifa uliopo nchini kwani ni jukumu la kila mtanzania wakiongozwa na viongozi wa dini.
