Benki Ya Duinia Kuikopesha Tanzani Dola Milioni 350 Kupanua Bandari Ya Dar

 BENKI ya Dunia imekubali kuikopesha Tanzania fedha kwaajili ya miradi mbalimbali ya maendeleo ukiwemo mkopo wa Dola Milioni 350 kwa ajili ya Mradi wa Upanuzi wa Bandari ya Dar es salam.
Waziri wa Fedha na Mipango, Dokta Philip Mpango, amewaambia waandishi wa Habari mara baada ya kumalizika kwa Mazungumzo kati yake na Makamu wa Rais wa Benki ya Dunia anaye shughulikia Kanda ya Afrika, Mhe. Makhtar Diop, Makao Makuu ya Wizara ya Fedha na Mipango Jijini Dar es salaam.

Amesema kuwa kukamilika kwa upanuzi wa Babdari hiyo kutasaidia kuongeza ubora wa huduma zinazotolewa na Bandari hiyo hatua itakayo chochea ukuaji wa  uchumi wa nchi.

Kwa upande wake Makamu wa Rais wa Benki ya Dunia anayeshughulikia Kanda ya Afrika Mhe. Makhtar Diop, amesema kuwa Benki yake imefurahishwa na hatua zinazochukuliwa na Serikali ya awamu ya tano katika kukuza uchumi na kwamba Benki hiyo itaendelea kushirikiana na serikali kuhakikisha kuwa malengo yaliyokusudiwa yana fikiwa kwa haraka

Ameishauri Serikali kuongeza ushirikiano kati yake na Sekta Binafsi katika kuchochea  biashara na uwekezaji pamoja na kutupia jicho sekta ya kilimo kwa kuboresha uzalishaji wa mazao ya kilimo na mifugo pamoja na kuongeza thamani ya mazao hayo ili kuwawezesha wananchi wengi zaidi kuondokana na umasikini na kuchochea uwekezaji katika sekta hiyo
Mpya zaidi Nzee zaidi