Na. Ahmad Mmow.
Mkuu wa wilaya ya Kilwa mkoa wa Lindi,Christopher Ngubiagai amemuagiza mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya wilaya ya Kilwa,amsimamishe kazi mganga mkuu wa hospitali ya wilaya hiyo,Vitalis Katalyeba ilikupisha uchunguzi kutokana na tuhuma mbalimbali zinazomkabili katika utendaji wake.
Ngubiagai alitoa agizo hilo jana akiwa katika kituo cha afya cha Tingi alipopitia kuangalia utekelezaji wa agizo lake kwa shirika la umeme (TANESCO) la kushugulikia changamoto ya umeme katika kituo hicho.Ngubiagai alimtaka mkurugenzi amsimamishe amsimamishe Dr Katalyeba sambamba na kuunda tume itakayo mshirikisha mganga mkuu wa mkoa ili kuchunguza ukweli wa tuhuma na malalamiko yanayotolewa dhidi ya mtaalamu huyo.
Mkuu huyo wa wilaya ambae alitoa agizo hilo baada ya kupokea malalamiko kutoka kwa baadhi yavwananchi na watumishi wa kituo hicho,alisema tuhuma anazotuhumiwa nazo hazivumiliki.Hivyo kwa kuzingatia taratibu,kanuni na sheria za utumishi na utawala bora anamtaka mkurugenzi amuweke pembeni ili uchunguzi upite."Natambua madaktari na wauguzi wanazo taratibu zao na mara zote huwa hawapendi kusema ukweli wanasema unawaingilia,lakini katika hili ni vigumu kuvumilia.Maana umuhimu na thamani yao nikwasababu ya kuwahudumia wananchi lakini kama mtu anashindwa kufanya hivyo inakuwaje asimbiwe au kuwajibika,"alihoji Ngubiagai.
Sambamba na kumuagiza mkurugenzi achukue hatua hiyo, pia amemuomba mganga mkuu wa mkoa wa Lindi kwa nafasi yake na kwakuzingatia taratibu,kanuni na sheria achunguze na kujiridhisha na kisha achukue hatua stahiki kwa Katalyeba iwapo mambo anayotuhumiwa na ayolalamikiwa ni yakweli."Huyo anazijua taratibu zao, achunguze na atueleze kama mambo yanayofanywa na daktari huyu ni sawa na taaluma yake,namajibu ya uchunguzi tunayataka,"akisema.Ngubiagai aliyataja baadhi ya mambo yanayotakiwa kupatiwa majibu kwanini amewahamisha watumishi watano wa kituo hicho kwa mkupuo.
Ikiwa ni muda mfupi tu tangu baadhi yatumishi kueleza tatizo la umeme lililokuwa linasababisha nyakati fulani wajawazito kujifungulia kwa kutumia mwanga wa tochi, kuwanyanyasa baadhi watumishi waidara wa idara hiyo,nakubwa kubwa kuliko yote ni sababu ya kifo cha mwanafunzi wa darasa la pili wa shule ya msingi Miteja aliyefia katika kituohicho baada ya kuchelewa kukimbizwa katika hospitali ya wilaya.Ikielezwa kuwa mganga mkuu huyo hakutoa ushirikiano na muuguzi wa kituo hicho.Badala yake alimdharahu na kumueleza kuwa hakusitahili kujulishwa na yeye.
Hivyo alipeleka gari saa 10 alasiri wakati mtoto huyoakiwa amefariki.Japokuwa taarifa hizo alipewa saa nnebasubuhi.Awali mmoja wa wawaugzi wakituo hicho,Mwanaisha Amanzi,pamoja na kumshukuru mkuu huyo wawilaya kutokana kumalizika kwa changamoto ya umeme katika kituo hicho lakini kitendo chake cha kumueleza tatizo hilo limemjengea uadui na mkuu wake wa idara.Kwasababu analaumiwa kwa kueleza tatizo hilo kwake na mbele ya waandishivwa habari."DC mimi nasakamwa hata nilipo muomba gari kwa ajili yule mwanafunzi akiyefariki hakunipa ushirikiano,aliliishia kuniita kwa jina langu,Amanzi, Amanzi,Amanzi, Tingi mnamatatizo sana,kwani huyo mgonjwa anaumri gani,nilipomtajia anamika tisa akaniambia aliesitahili kumpa taarifa hiyo sio mimi bali muuguzi wa zahanati ya Miteja.
Alikatata simu na hata nilipompigia tena alikuwa hapokei hadi nilipo tumia simu ya mtu mwingine nakumueleza huyo mgonjwa amefariki kwahiyo kama ataleta gari ni kwaajili ya kusafirisha maiti," alisema Mwanaisha.Mlezi wa mtoto aliyefariki (Matilda Pinda,miaka tisa), Magreth Nguli aliunga mkono maelezo ya Mwanaisha kuhusu mazingira ya kifo cha mtoto Matilda."Kila alichokuwa anafanya huyo muuguzi na majibu ya huyo daktari tulikuwa tunasilikia,hata alipoacha kupokea simu yake tulikuwa tunaona na ndipo tulimpa simu nyingine alipompigia slipokea,uhenda alidharahu kwakuwa aliyekuwa anaumwa ni mtoto.Kwasababu alipotajiwa umri wa mgonjwa alikata simu kabisa," alisema Magreth.
Mganga mfawidhi wa Kituo hicho,Christopher Kunde alikiri kuwa kuwa watumishi wa tano wakituo hicho akiwamo Mwanaisha wamepata barua za uhamisho.Alisema ingawa barua hizo zimeeleza ni uhamisho wa kawaida lakini alishangaa kuona wanahamishwa wengi kwa mpigo.
Tena ni muda mfupi tu baada ya kuibuliwa tatizo la umeme na maji katika kituo hicho.Kwa upande wake,mganga mkuu huyo, Dr Katalyeba alipoulizwa kwa njia ya simu na mwandishi wa habari hii kuhusu tuhuma na malalamiko hayo alisema yeye sio msemaji wa halmashauri ya wilaya.Hivyo aulizwe yeye kwasababu utarati,kanuni na sheria inataka hivyo.
Nayeye anaheshimu mambo hayo.Hata alipoambiwa na kukumbishwa tuhuma nyingi zimemlenga yeye binafsi,mganga Dkt Katalyeba aclishikilia msimamo wake wakumtaka mwandishi awasiliane na DED wa Kilwa.Juhudi za kumpata DED wa Kilwa,Zabron Bugingo hazikuweza kufanikiwa.Baada ya simu yake kutokuwa hewani.MWISHO.