Donald Trump apokelewa kwa maandamano

Waandamanaji katika mji mkuu wa Uhispania Madrid wakiwa na mabango ya kumtaja Barrack Obama kama 'matumaini na Donald Trump ''Chuki.

Maandamano makubwa kutoka kwa makundi ya wanawake dhidi ya Donald Trump yamekuwa yakifanyika Australia,New Zealand na Japan.

Maandamano makubwa zaidi yamefanyika mjini Sydney, Australia,ambako karibu watu elfu tatu wameandamana kuelekea katika ubalozi wa Marekani nchini humo. Waandamanaji

wanampinga Bw. Trump hasa juu ya madai ya mwenendo wake wa kuwakosea heshima wanawake.

Nchini Marekani pia kumeshudiwa katika mji wa Washington wakati wa hafla ya kuapishwa kwa Donald Trump kuwa Rais wa 45 wa taifa hilo.

Polisi mjini huo walilazimika kutumia gesi ya kutoza machozi kwawatawanya waandamanaji huku baadhi yao wakiharibu magari na na hata kuyachoma moto.

Maadamano mengine mia saba sawia na hayo yanapangwa kufanyika leo katika miji mingine mikuu Duniani.


JIUNGE NASI KATIKA
INSTAGRAM @Muungwanablog

FACEBOOK @Muungwana Blog

YOUTUBE @Muungwana Tube

BOFYA HAPA KU-INSTALLAPP YA MUUNGWANA BLOG ILI UPATE URAHISI KUZISOMA HABARI ZOTE KWA WAKATI.
Mpya zaidi Nzee zaidi