Baadhi ya Wananchi katika eneo la Vingunguti jirani machinjio ya Vingunguti jijini Dsm wamedai kuwa eneo la dampo la hekari nane ambalo wanadai lilitengwa kwa ajili ya vijana watengeneza majiko na Viwanda vidogo pamoja na mamalishe limebinafshwa kwa mwekezaji kinyume na matumizi ya yaliyokusudiwa.
Wakizungumza na Chanel ten wananchi hao wakiongozwa na mwenyekiti wa kamati inayofatilia eneo hilo Bw,Philipo Mpemba wamedai kuwa Eneo hilo la Hekali nane lilikuwa eneo la kutupa taka kwa wakazi wa Vingunguti na Tabata ambapo amedai mara kadhaa viongozi waliotembelea walikubaliana kutenga eneo hilo kwa ajili ya wajasiliamali.
Viongozi hao wamedai kuwa suala hilo mara kadhaa wameshaliwasilisha kwa m/kiti wa serikali za mtaa,halmashauri ya manispaa ya ilala lakini bado hawajafanikiwa,huku wananchi zaidi ya 40 wakitakiwa kulipwa fidia ambapo vijana wajasiliamali watengenezaji na wauza majiko zaidi ya mia 400 wakizaagaa kwa kukosa eneo la kufanyia biashara.