Gereza laomba wafungwa zaidi

Mbeya. Mkuu wa Gereza la Kilimo Songwe,  Lyzeck Mwaseba ameiomba Serikali kulipatia wafungwa wengi na pembejeo ili kuongeza uzalishaji.

Miongoni mwa pembejeo hizo ni majembe, matrekta na mitambo mingine ya kilimo.

Mwaseba  aliwasilisha ombi hilo mbele ya Kamati ya Bunge ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama iliyotembelea gereza hilo ikiambatana na Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Hamad Masauni.Ziara hiyo ililenga kujionea uzalishaji wa mahindi unaofanya na wafungwa.

“Gereza hili lina ukubwa wa hekta 2,170, lakini hivi sasa zinalimwa eka 250 kutokana na kuwapo wafungwa 165 tu ambao ni wachache,’’ alisema.

JIUNGE NASI KATIKA
INSTAGRAM @Muungwanablog

FACEBOOK @Muungwana Blog

YOUTUBE @Muungwana Tube

BOFYA HAPA KU-INSTALLAPP YA MUUNGWANA BLOG ILI UPATE URAHISI KUZISOMA HABARI ZOTE KWA WAKATI.
Mpya zaidi Nzee zaidi