KAIMU Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam ambaye pia ni Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Ali Hapi amekabidhi mifuko 100 ya saruji ambayo ni sawa na tani tano kwa Jeshi la Polisi Wilaya ya Kariakoo.
Hapi alikabidhi mifuko hiyo jana baada ya kutembelea makazi ya polisi wanaoishi Kituo cha Polisi Msimbazi, ambapo zinaishi familia 72 na kukuta jengo hilo lenye ghorofa nne ni chakavu, limejengwa tangu enzi ya mkoloni.
Alisema ametoa msaada huo kwa kuwa jeshi la polisi linafanya kazi kubwa na nzuri usiku na mchana, kwa kulinda raia na mali zao, hivyo nalo linapaswa kuangaliwa kwa jicho la karibu.
“Tumekuwa hodari wa kuwalaumu polisi, lakini ukweli ni kwamba wamekuwa wakijitahidi kutulinda na kulinda mali zetu. Mimi nimezaliwa katika kambi ya polisi na nilipofika katika jengo hili nimeguswa na kuamua kuchangia simenti ambayo itafanya ukarabati wa jengo zima katika maeneo yote yaliyoharibika,” alisema Hapi.
Aliitaka jamii kuliangalia jeshi hilo ili kuhakikisha wanakaa katika mazingira mazuri ili nalo liendelee na kasi ya kuwalinda wananchi na mali zao.
Alitaka viongozi kusimamia mifuko hiyo, iliyotolewa ili ikafanye kazi iliyokusudiwa, endapo itapungua aliomba apewe taarifa ili aangalie njia ya kuongeza.
Alisema jengo hilo, halijawahi kufanyiwa ukarabati tangu lilipojengwa enzi ya mkoloni, jambo ambalo linaweza kuleta athari katika siku za mbele endapo litaporomoka.
Mrakibu wa Polisi, Jasson Ibrahim ambaye ni Mkuu wa Polisi Wilaya ya Kariakoo, alishukuru kwa msaada huo uliotolewa anaamini utatumika kwa malengo yaliyokusudiwa.