Huyu atakuwa Kiongozi wa kwanza kukutana na Rais Trump

Theresa May kukutana na Trump Ijumaa ijayo

Waziri mkuu wa Uingereza,Theresa May anatarajia kukutana na Rais wa Marekani Donald Trump Ijumaa ijayo.

Theresa May atajadili kuongeza uhusiano maalumu baina ya Uingereza na Marekani pale atakapokuwa mmoja kati ya viongozi wa kwanza kukutana na Rais Trump wiki ijayo.

Kwa mujibu wa habari Bi Theresa aliongeza kwa kusema kuwa anatarajia kutapatikana uwezekano wa kuwa na makataba mpya wa biashara na nchi ya Marekani.

Hali kadhalika waziri mkuu wa Uingereza alisema atagusia masuala ya NATO na udhibiti dhidi ya magaidi katika mkutano huo.

Bwana Trump amekwisha anza kazi rasmi kama Rais wa 45 wa Marekani.
Mpya zaidi Nzee zaidi