Jinsi Mexico itakavyolipa gharama ya ujenzi wa Ukuta baina yake na Marekani

Kashfa ya fedha ya ujenzi wa ukuta baina ya Marekani na Mexico

Baada ya rais mpya wa Marekani kutia saini mradi wa kujenga ukuta mpakani mwa Mexico,sasa mjadala mkali wa fedha za kugharamia mradi huo wazuka baina ya serikali hizo mbili .

Baada ya mjadala wa muda mrefu kuhusu gharama za ujenzi wa ukuta huo ,rais Trump aliandika ujumbe kupitia akaunti yake ya Twitter;

"Ikiwa serikali ya Mexico haina nia ya kutoa fedha za kugharamia ujenzi wa ukuta basi ni sahihi kusitisha mkutano unaotarajiwa ."

Viongozi wa Mexico hata hivyo wameonekana kushangazwa na uamuzi wa bwana Trump kusitisha mkutano baina yake na rais Nieto Januari 31 jijini Washington .

Katika taarifa yake rais wa Mexico Enrique Pena Nieto, alifahamisha kuwa ;

"Nilifanya mazungumzo na White House asubuhi ya leo na kumuarifu rais wa Marekani kuwa sitohudhuria mkutano wa Washington wa Januari 31."

Katika taarifa nyingine ya Trump kumjibu Nieto alisema kuwa yeye na Pena Nieto walikubaliana kwa pamoja kusitisha mkutano huo wa Washington.

Kwa upande mwingine msemaji wa ikulu ya Marekani Sean Spicer amefahamisha kuwa Trump ana mipango ya kutoza kodi ya asilimia 20 kwa bidhaa zote zinazoingizwa Marekani kutoka Mexico na kutumia fedha hizo kugharamia ujenzi wa ukuta .
Mpya zaidi Nzee zaidi