Kaka Mtu Akamatwa kwa Kumbaka na Kumtoa Usichana Dada Yake wa Miaka 4..!!!

  YAWEZEKANA ikawa  ni  moja ya  sababu ya  mvua  kuchelewa kunyesha  mkoani Iringa tofauti  na  ilivyozoeleka  miaka  mingine  ni  kutokana na laana kama hizi  baada  ya kikosi  maaalum kinachoongozwa   mkuu  wa  wilaya ya Iringa  Richard Kasesela  kwa  kushirikiana na OFM kufanikiw kumkamata  kijana Emmanuel Mkiwa  (19) kwa tuhuma  za kumbaka mara kwa
mara mdogo wake  wa miaka (4)

Afisa  maendeleo ya  jamii Manispaa   ya  Iringa  Josephina Mwaipopo  akiwa na mtoto aliyebakwa

Imedaiwa kuwa kijana  huyo  ambae  ni mwenyeji  wa mtaa  wa Omary  Matrekta kata ya  Mtwivila  katika  Manispaa ya  Iringa alikuwa akiishi nyumba  moja na babake pamoja na wadogo  zake watatu  wawili  wa  kiume na mmoja ni  mtoto   huyo  wa  miaka 4  ambaye alitelekezwa  na mamake  mzazi kutokana na mambo ya  kifamilia kati  yake baba  wa  mtoto .

Mashuhuda wa  tukio   hilo  lililotokea January 16 majira ya  saa 2 usiku walimweleza  mwandishi  wa  OFM  Iringa  kuwa kijana   huyo mara  kwa mara  alikuwa  akimbaka  mdogo wake  huyo  ambae baba  mmoja  na mama tofauti kabla  ya  mtoto   huyo kuwaeleza majirani   kuwa kakake  huyo amekuwa akimkandamiza na  kijiti sehemu  zake  za  siri (Akimbaka)

Kutokana na  maelezo ya  mtoto   huyo ndipo taarifa  za  raia  wema  hao zilipofikishwa kwa mkuu  wa  wilaya  na OFM na  kuamua  kufika  katika eneo la  tukio na  kufanikiwa  kumkamata kijana   huyo  na baba mzazi wa  watoto  hao  Shukuru Mkiwa kwa malezi mabaya  ya  watoto.

Akizungumza baada ya  kukamatwa  kwa  kijana   huyo  mkuu  wa  wilaya ya  Iringa Richard  Kasesela   pamoja na  kuwashukuru raia wema  kwa  kufikisha taaarifa  ya  kunyanyaswa  kwa mtoto   huyo  bado  alitoa wito kwa wananchi  wengine  ambao  wanataarifa  za  kunyanyaswa  kwa  mtoto yeyote  katika  wilaya ya  Iringa  kutoa taarifa  ili  wahusika wakamatwe  na  kufikishwa  katika  vyombo  vya sheria.

Kasesela alisema  kuwa uchunguzi   uliofanywa baada ya  vipimo katika  Hospitali ya  Rufaa ya  mkoa  wa  Iringa umeonyesha mtoto   huyo kashaondolewa usichana wake   na  hivyo kulazimika  kulazwa  kwa  matibabu katika Hospitali   hiyo huku akiahidi kumsaidia mtoto  huyo  kumsomesha .

Alisema kuwa yawezekana  moja ya  sababu ya  mvua  kuchelewa  kunyesha katika mkoa  wa Iringa  ni  pamoja  na matukio ya  kinyama kama haya ya ubakaji  watoto na  kuwa  hatakubali kuona mbakaji  anaendelea   kuishi uraiani wilaya ya  Iringa kwani tayari  mkuu  wa  mkoa  wa  Iringa Amina Masenza  kupitia  kikao  cha makati ya  ushauri ya  mkoa (RCC) aliagiza wabakaji wote wasakwe kwa udi na uvumba na yeye ameanza
kutekeleza agizo hilo.

Japo alisema alishangazwa  na hatua ya baba  mzazi wa  kijana  huyo kumficha mbakaji ndani na  kudanganya  kuwa  hayupo wakati  kijana wake  alikuwepo  ndani hivyo  mzazi  huyo  kukamatwa pamoja na kijana wake yeye kwa  kosa la  kumchifa  mharifu  na kijana wake kwa kosa la ubakaji .

“Hiki  ni  kikosi  kamili  ambacho kitaendelea  kuendesha  misako  mbali mbali kwa kushirikiana na oparesheni  Fichua Maovu (OFM) ya Global Publishers hivyo kwa  yeyote  anayejua  wapi  mtoto anafanyiwa vitendo  vya kikatili piga  simu hii mwandishi wa OFM Iringa 0754 026 299 tutakufikia ulipo na
kuchukua  hatua”

Jeshi la  polisi  mkoa  wa Iringa  kupitia kwa  kamanda wa  polisi  mkoa (RPC) Julius Mjengi limethibitisha  kukamatwa kwa mtuhumiwa   huyo na  kuwa baada ya  upalelezi  atafikishwa mahakamani  huku  likiwataka  wananchi  kuendelea  kufichua  waharifu  zaidi

JIUNGE NASI 
 INSTA@MUUNGWANABLOG ,FB@MUUNGWANABLOG,YOUTUBE @MUUNGWANA TUBE, BOFYA HAPA KU-INSTALL APP YA MUUNGWANA BLOG ILI UPATE URAHISI KUZISOMA HABARI ZOTE KWA WAKATI.