Kamati inayoshughulikia mgogoro wa ardhi Loliondo yashindwa kutoa maamuzi

Wajumbe Wa kamati inayoshughulikia mgogoro  wa ardhi katika pori tengefu la Loliondo wameshindwa kutoa maamuzi   ya  hatma  ya  tatizo  hilo  baada ya hoja zilizowasilishwa na  wataalam,wawekezaji na wananchi  kuonekana kuwa   zinazopingana na sheri zilizopo na pia kutokuwa  na  maslahi  mapana  kwa  wañanchi na taifa kwa ujumla.

Miongoni mwa mwa hoja zilizotajwa kuleta mkanganyiko ni pamoja na  kukiukwa kwa sheria zinazosimamia pori tengefu ,uwekezaji ,na  matumizi bora ya ardhi na pia  haki za wananchi.

Kutokana na hali hiyo mwenyekiti wa kamati hiyo iliyoundwa  kutekeleza  agizo  la  Waziri  Mkuu  Mh  Kassim  Majaliwa  Bw Mrisho Gambo  amelazimika  kuunda kamati nyingine ya wataalam ,wanasheria, wawekezaji  na  wananchi   ya  kushughulikia changamoto  zilizojitokeza na  kutoa  tena  mapendekezo.

Pamoja  na  changamoto hizo  baadhi ya wajumbe  wa  kamati  ya  kutatua  mgogoro  huo  unaofukuta  kwa  zaidi ya miaka  20 wamesema   hatua  iliyofikiwa ni  nzuri hasa kutokana na  ushirikishaji  mkubwa  wadau  wanaoguswa na mgogoro huo wakiwemo  wananchi  ambao  kwa  sasa  wameshirikishwa  ipasavyo.
Mpya zaidi Nzee zaidi