Kinachoendelea kwasasa, wakati mgodi wa Buzwagi ukielekea kufungwa

Related imageMgodi wa dhahabu wa Acacia Buzwagi, wilayani Kahama, mkoani Shinyanga, umezindua kampeni maalumu upandaji miti inayojulikana kwa jina la Wakia moja mti moja yenye lengo la kupanda miti milioni moja na laki sita katika kipindi cha miaka miwili, ikiwa ni utekelezaji wa mkataba katika zoezi la kuelekea kufunga shughuli za uzalishaji za mgodi huo na kurejesha uoto wa asili wa mazingira.
Mbele ya lango kuu la mgodi wa dhahabu wa ACACIA Buzwagi, Mkuu wa wilaya ya Kahama, Fadhili Nkurlu anazindua kampeni hiyo kwa kushiriki zoezi la kupanda miti ambapo anazikumbusha halmashauri zote za kahama mji, Ushetu na Msalala kutekeleza zoezi hilo kwa lengo la kuboresha mazingira ya wilaya hiyo.

Akizungumzia kufungwa kwa shughuli za uchimbaji katika mgodi huo wa dhahabu wa Buzwagi, Mhandisi Asa Mwaipopo anasema.

Mgodi wa dhahabu wa buzwagi ulianza shughuli za uchimbaji madini ya dhahabu mwaka 2008 na unatarajia kufunga shughuli hizo desemba mwaka huu na baadae kuendelea na uzalishaji kwa mawe yaliyochimbwa katika kipindi cha miaka miwili mingine.
Mpya zaidi Nzee zaidi