MICHUANO ya Kombe la Shirikisho (FA), huwenda ikaingia doa baada ya kuwapo kwa taarifa za matumizi mabaya ya fedha za udhamini wa mashindano hayo zinazotolewa na wadhamini.
Kalenda ya Shirikisho la soka Tanzania (TFF) inaonyesha mwisho wa wiki hii kunapasa kuwapo kwa michezo ya kombe hilo la Shirikisho lakini habari za ndani ambazo Nipashe imezipata zinadai michezo hiyo haitakuwapo kutokana na wadhamini kutotoa sehemu ya fedha za udhamini wao wa mashindano hayo.
Hata hivyo mmoja wa viongozi wa TFF aliiambia Nipashe kuwa fedha ambazo hazijamalizwa na wadhamini wa mashindano hayo ni ndogo na haziwezi kuzuia michezo hiyo kufanyika.
"Sehemu kubwa ya fedha za udhamini wa mashindano haya zimeshatolewa na wadhamini, kinachoonekana ni kuwapo kwa matumizi tofauti ya fedha hizi," alisema kiongozi huyo ambaye hakutaka jina lake kutajwa gazetini.
Alisema hilo linaweza likatia doa ushirikiano uliopo baina ya wadhamini wa mashindano hayo na TFF.
Alipotafutwa Ofisa habari wa TFF, Alfred Lucas kuzungumzia ratiba ya michuano hiyo ya Kombe la Shirikisho alijibu hana taarifa.
"Sijawasiliana na wahusika, hivyo siwezi kusema chochote juu ya ratiba ya kombe hilo la Shirikisho," alisema Lucas.

JIUNGE NASI KATIKA
YOUTUBE @Muungwana Tube
BOFYA HAPA KU-INSTALLAPP YA MUUNGWANA BLOG ILI UPATE URAHISI KUZISOMA HABARI ZOTE KWA WAKATI.