MBUNGE wa jimbo la Ubungo, Saed Kubenea, leo Jumapili, ameungana na viongozi waandamizi wa upinzani nchini, Edward Lowassa na Maalim Seif Sharif Hamad, kumpigia kampeni mgombea ubunge jimbo la Dimani, Unguja,

Akizungumza na MwanaHALISI Online, Kubenea alisema, “ninakwenda Unguja kutafuta mbunge. Nakwenda kuongeza nguvu. Nakwenda Unguja, kushinda.”
Kubenea, mmoja wa wabunge machachari wa upinzani nchini anasema, ameamua kwenda Unguja ili kusaidia harakati za ukombozi kwa kuhakikisha Chama cha Wananchi (CUF), kinashinda katika uchaguzi huo.
Uchaguzi mdogo wa Dimani Unguja, unafanyika kufuatia aliyekuwa mbunge wa jimbo hilo, Hafidhi Aly Twahir, kufariki dunia mwishoni mwa mwaka jana mjini Dodoma.