Kuwait imetoa adhabu ya kifo na kunyonga watu saba wenye makosa tofauti.

Kati ya walionyongwa ni raia wawili kutoka Kuwait,wawili kutoka Misri,mmoja wa Bangladesh,mmoja wa Ethiopea na mwingine kutoka Ufilipino.
Kati ya raia wawili walionyongwa mmoja wao Faisal Abdullah al-Jaber al-Sabah anatokea familia ya Kifalme iliyotawala Kuwait miaka ya nyuma.
Faisal Abdullah al-Jaber al-Sabah amepewa adhabu ya kifo baada ya shutuma za kumuua mpwa wake mwaka 2010.
Adhabu ya kifo imekuwa ikifutwa katika baadhi ya nchi duniani kutokana na uzito wa adhabu hiyo.