Machinjio ya ng’ombe Shinyanga Yalalamikiwa

screen-shot-2017-01-08-at-11-27-56-am

Wananchi wa manispaa na mkoa wa Shinyanga, wameitaka serikali kuiondoa machinjio ya Ng’ombe iliyopo katikati ya mji huo, iliyojengwa tangu mwaka 1940, kwa kuwa inaharibu mazingira kwa kutiririsha maji machafu yenye harufu mbaya kwenye makazi ya watu hivyo kuhatarisha afya za wakazi kwa hofu ya kukumbwa na magonjwa ya mlipuko kama kipindupindu, na kuhara damu.

Wakiwasilisha kero zao katika mkutano wa hadhara uliondaliwa na Mkuu wa wilaya ya Shinyanga, Josephine Matiro, kusikiliza kero mbalimbali zinazowakabili wananchi hao, wamesema machinjio hayo yamekuwa yakihatarisha afya za wakazi wa maeneo hayo.

Kufuatia hali hiyo Mkuu huyo wa Wilaya akalazimika kwenda kukagua machinjio hayo ambapo pamoja na mambo mengine amesema serikali imetenga kiasi cha sh. Bilioni 8, kwa ajili ya ujenzi wa machinjio mapya.

Awali akijibu kero za wananchi Josephine matiro ameagiza watendaji wa idara mbalimbali kuzifanyia kazi kero hizo na kuzitolea majibu katika kikao cha kila mwezi kitakachokuwa kikifanyika.
Mpya zaidi Nzee zaidi

Popular Items

Kilimo cha Bamia