Wafugaji 50 walionusurika na njaa Warejeshwa wilayani Rufiji

screen-shot-2017-01-08-at-4-38-30-pm

Wafugaji hamsini walionusurika kufa njaa kwenye pori la Selous wakati wakisafiri na mifugo yao kutoka wilayani Rufiji Mkoa wa Pwani kwenda Morogoro wamerejeshwa na serikali wilayani humo, hatua iliyoibua furaha walipokutana na ndugu zao.

Hafla maalum ya kuwapokea wafugaji hao iliandaliwa mjini Utete yalipo makao makuu ya wilaya ya Rufiji, ambapo Katibu Mkuu wa Chama cha Wafugaji Tanzania Bw. Makoye Maghembe aliyekuwa mgeni rasmi, alilaani matamko ya viongozi wa serikali yanayosababisha maisha ya wafugaji kutawaliwa na hofu.

Hata hivyo Bw. Maghembe na viongozi wengine wa serikali waliohudhuria hafla hiyo walisikitishwa kuona kati ya watoto wadogo 15 wenye umri wa kati ya miaka minane na kumi na minne, waliokuwa miongoni mwa wanusurika, hakuna hata mmoja aliyewahi kupelekwa shule na kuitaka jamii ya kifugaji kubadilika na kuthamini elimu kupitia utajiri huo wa mifugo.

Katika tukio hilo, jumla ya ng’ombe 1828, Kondoo 215, Mbuzi 21, Punda 4 na Mbwa 3 walipotea, ambapo tayari ng’ombe 800 wamepatikana na juhudi za kutafuta mifugo mingine inaendelea.
Mpya zaidi Nzee zaidi

Popular Items

Kilimo cha Bamia