MAFUNDI watatu wa umeme wametiwa mbaroni kwa tuhuma za kukusanya zaidi ya Sh. 700,000 kutoka kwa wananchi wa Kijiji cha Mbinga Mhalule Wilaya ya Songea kwa madai ya kuwasimikia nguzo za umeme wa Rea.
Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Ruvuma, Zuberi Mwombeji, alisema tukio hilo lilitokea Desemba 24, mwaka jana.
Kamanda Mwombeji aliwataja watuhumiwa hao kuwa ni Gwido Mwalongo (36), mkazi wa Njombe, Innocent Mwakisyala (27) na Philbert Soko (34), wote wakazi wa Lizaboni Manispaa ya Songea.
Alifafanua kuwa kukamatwa kwa watuhumiwa hao kulitokana na malalamiko ya wananchi kwamba watuhumiwa hao wamekusanya kiasi hicho cha fedha wakidai watawasimikia nguzo za kupitisha umeme kijijini hapo.
Kamanda Mwombeji alisema polisi walipokwenda eneo la tukio, wananchi walilizingira gari wakitaka warudishiwe fedha zao walizotoa kwa watuhumiwa hao.
Alisema hali ilibadilika ghafla baada ya wananchi hao kutishia kuwadhuru polisi na watuhumiwa.
Kamanda Mwombeji alisema kutokana na hali hiyo, ndipo walipowalazimisha watuhumiwa hao kuwarejeshea wananchi fedha zao huku stakabadhi za malipo hayo zikichukuliwa na polisi kama ushahidi.
Kwa mujibu wa Kamanda Mwombeji, kaya 37 za kijiji hicho cha Mbinga Mhalule, kila moja ilichangishwa Sh. 20,000 kwa ajili ya kusimikiwa nguzo kwenye eneo la kaya husika.
Hata hivyo, Kamanda Mwombeji alifafanua kuwa baada ya kuwahoji mafundi umeme hao, ilibainika kuwa wametoka kampuni moja ya kuunganisha umeme majumbani ya mjini hapa.
Alisema watuhumiwa hao wanaendelea kuhojiwa na polisi na wanatarajiwa kufikishwa mahakamani mara tu mahojiano hayo yatakapokamilika.
Kaimu Meneja wa Shirika la Umeme nchini (Tanesco) Mkoa wa Ruvuma, Mhandisi John Kiduko, alipohojiwa na Nipashe ofisini kwake jana kuhusiana na mafundi umeme hao waliokamatwa, alisema" kwa muda mrefu wamekuwa wakipata malalamiko kuwa kuna watu wamekuwa wakipita kwenye vijiji wakidai kuwa wametumwa na shirika la umeme Tanesco kukusanya fedha kwa watu wanaotaka kusimikiwa nguzo jambo ambalo alieleza si la kweli.
Kiduko alisema alipata taarifa za watuhumiwa hao Desemba 24, mwaka jana kuwa kuna wafanyakazi wa Tanesco wamefika katika kijiji hicho na wanakusanya fedha kwa ajili ya kazi ya kuwasimikia nguzo za umeme.
Alisema baada ya kupata taarifa hizo, aliwasiliana na vyombo vya dola na watuhumiwa hao wakatiwa mbaroni.
Aidha, alisema mafundi hao hawakutumwa kukusanya fedha kama walivyofanya na kwamba kitendo walichofanya wameichafua Tanesco.
Source: Nipashe