Malkia Elizabeth akosa ibada ya mwaka mpya

Malkia wa Uingereza augua homa kali

Malkia wa Uingereza kwa mara nyengine amekosa kuhudhuria ibada ya kuadhimisha mwaka mpya katika kanisa la Sandringham kutokana na homa makali.

Malikia Elizabeth pia alikosa ibada ya siku kuu ya Krismasi nyumbani kwake huko Norfolk na hajaonekana hadharani kwa siku 12 sasa.

Msemaji wa Kasri la Buckingham amesema kuwa malkia anaendelea kupata nafuu.

Yeye na Duke wa Edinburgh walichelewa kwa likizo yao ya Krismasi kwa siku moja mnamo Disemba 22, na kusafiri kwa kutumia ndege aina ya helikopta badala ya treni kutokana na homa.

Binti Mfalme Anne aliulizwa vile mamake alivyokuwa akiendelea alipowasili katika kanisa ambapo alijibu vyema.
Mpya zaidi Nzee zaidi